Jumatatu , 13th Apr , 2015

Msanii wa filamu Desmond Olusola Elliot wa Nigeria, ameshinda kiti cha uwakilishi wa jimbo la Surulere lililopo nchini humo, baada ya kuwania nafasi hiyo akikabiliana na mpinzani wake Bayo Smith wa chama cha Peoples Democratic Party.

muigizaji nyota wa filamu nchini Nigeria Desmond Elliot

Staa huyo kabla hata ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo, alionekana na wapambe wake wakisherekea ushindi kutokana na uhakika uliojengwa na ushawishi na umaarufu mkubwa kutoka fani yake ya uigizaji.

Staa huyo ambaye sasa anaanza kuonja utamu wa siasa, alijiunga na chama cha All Progressives Congress (APC), akiweka wazi kuwa hatua yake hiyo ni kutokana na hamasa kutoka kwa wanasiasa maarufu wakiwepo magavana Godswill Akpabio na Babatunde Raji Fashola.