Jumamosi , 25th Apr , 2015

Katika kipindi hiki ambacho Tanzania inakabiliwa na janga la mauaji ya walemavu wa Ngozi (Albino), msanii wa muziki Danny Msimamoa ameamua kufikisha ujumbe kukemea tatizo hilo kupitia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina Mimi kama Wewe.

Sugu, Danny Msimamo na Adili Chapakazi

Danny Msimamo ambaye ni msanii mkongwe katika game ya michano Bongo, amesema kuwa rekodi hiyo ambayo ameifanya kwa hisia nzito, ina lengo la kuendelea kusisitiza kwa jamii kuwa na usawa, na kuchukulia Albino kama vile walivyo binadamu wengine.

Staa huyo amesema kuwa, mipango ya video ya kazi hiyo ipo mezani kwa sasa akijaribu kushirikisha baadhi ya wadau ili kuwakilisha ujumbe huo pia kwa kupitia picha baada ya kukamilisha rekodi hiyo iliyofanywa katika studio za Noisemakerz chini ya producer DX.