msanii wa nchini Kenya Daddy Owen
Daddy Owen ameweka wazi kuwa, mpango huu utafanyika kupitia kampeni ambayo imepewa jina la 'Inua Dada' ambayo inatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika namna watoto wa kike wanavyochukuliwa na kuishi katika jamii.
Kampeni hii inakuwa ni sehemu nyingine ya shughuli nyingi za Daddy Owen katika kuirejeshea jamii shukrani kutokana na mafanikio anayoendelea kujipatia kila siku kupitia sanaa yake ya muziki.
Mbali na hilo hivi karibuni, Daddy Owen ameweka wazi ujio wa projekti kubwa kabisa itakayowahusisha wote kwa pamoja hivi karibuni.