Alhamisi , 5th Feb , 2015

Star wa muziki wa injili wa nchini Kenya, Daddy Owen pamoja na Papa Dennis tayari wamekwishatua Jijini London Uingereza kwa ajili ya shughuli ya upigaji picha za video ya kolabo yao ambayo inafahamika kwa jina "Foundation".

Wasanii wa muziki wa injili nchini Kenya, Daddy Owen na Papa Dennis

Kwa njia ya mtandao, mastaa hawa wameweka picha kuonesha mashabiki wao kuwa wamefika na wamejipanga sawa sawa kwa ajili ya kazi hiyo ambayo inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa kwa upande wa utayarishaji video za muziki nchini Kenya na Afrika Mashariki.

Katika safari hii mastaa hawa wameongozana na mdau mkubwa wa burudani nchini Kenya, Sadat Muhindi ambaye pia amekuwa na mchango mkubwa katika kusimamia kazi za msanii Papa Dennis.
..............................