Jumanne , 5th Mei , 2026

Msanii wa hip hop DaBaby amezua mjadala mkubwa baada ya kudai kuwa yeye ni bora kuliko kundi la marapa wanaojulikana kama “Big 3”, linaloundwa na Drake, Kendrick Lamar na J. Cole.

Kauli hiyo ilitolewa wakati wa mahojiano yake na Apple Music yaliyotolewa kupitia YouTube tarehe 24 Aprili, ambapo DaBaby alionyesha kujiamini kwa kiwango cha juu kuhusu uwezo wake katika muziki wa rap.

Katika mahojiano hayo, DaBaby alisisitiza kuwa tangu aanze safari yake ya muziki, amekuwa akijiona kama rapper bora zaidi, akieleza kuwa kauli hiyo si mpya kwake kwani amekuwa akiirudia mara kwa mara, hasa katika freestyle zake.

Kauli yake imeibua mjadala mkali mitandaoni, huku mashabiki wa hip hop wakigawanyika kuhusu nani anastahili kuitwa rapper bora zaidi kati ya wasanii hao. Wapo wanaomuunga mkono kwa kujiamini kwake, huku wengine wakisisitiza kuwa “Big 3” bado wana mchango mkubwa na ushawishi mkubwa zaidi katika tasnia ya muziki.

Kwa sasa, mjadala huo unaendelea kushika kasi, ukiakisi ushindani mkubwa uliopo ndani ya muziki wa hip hop duniani.