Ijumaa , 17th Jun , 2016

Msanii Cyril Kamikaze ameamua kumaliza mgogoro uliopo kuhusu wimbo wake mpya wa Cheza kidogo, alioshirikisha Raymond.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Cyril ameadika ujumbe mrefu na kuelezea ni jinsi gani ameumizwa na kauli ya Raymond kuwa ameamua kutoa wimbo huo sasa ili kupata kiki, ingawa alikiri kufanya kazi hiyo na yeye kabla hajawa maarufu.

Katika waraka huo Raymnd amesema ameamua kumaliza mgogoro huo kwa kutoipa promo tena nyimbo hiyo, na hata video ambayo alishaanza kuiandaa ameghailisha, na kuamua kuifanya kama bonus track kwa mashabiki.

"Nilishasahau kuhusu hili na nikaamua kukaa kimya kabisa nikiamini ni busara tu ila sababu imeendelea jana tena east africa acha niimalize tu....wakati tunaufanya huu wimbo tulifanya kwa furaha zote ,nawewe mwenywe ulijua huu wimbo utatoka radio bila hata wewe kujua kama unge kuja kua na hii KIKI unayo isema now, hata kwa majibu yako umekubali tumefanya collabo ,well najisikia vibaya now niki promote wimbo ambao mimi nawewe tuliufanya kwa love na ushirikiano mkubwa mpka kuisha alafu wewe unasema haukua na haja ya kuwepo kwenye collabo and pia unachukia watu wanao toa ngoma now kwasababu una kiki kama binadamu inaniumiza and inanipa hisia ya kulazimisha hili suala la huu wimbo CHEZA KIDOGO uendelee kusiskika wakati ni wazi umetaka nionekane naitaji sana jina lako na kiki yako ili huu wimbo uende au uhit wakati mimi naamini na niliamini tu huu ni wimbo mzuri bila hata kiki yako ndugu Raymond.. anyway maneno yasiwe mengi,sitaki ugomvi beef wala chuki na mtu kwa jambo ambalo mimi naliona dogo sana,na heshimiana na watu unaofanya nao kazi na bado safari yetu ndefu sana ki sanaa so Am calling it off ! Well huu wimbo sito ufanyia tena promo official na kama ushaenda au watu wame u download ni poa ni kama a bonus track kwa mashabiki one love ✌? na pia nimeingia gharama za kulipa video watu, arrangements zote nitazi samehe tu mwana ili upunguze hasira za watu kutoa nyimbo ulizo fanya nao kabla hujapata KIKI ikiwemo mimi kwa kusema tulikuwa wapi, maana hata kama ngoma inasubiri foleni ingetoka tu, ..Since majibu yenu yamejibiwa internet namimi najibu iwe hivi internet ,ki amani kabisa na kiroho safi no hard feelings..#finalkabisa" alichokiandika Cyril kamikaze.

Hapo jana baada ya Raymond kufanyiwa interview na eNews ya EATV, alikiri kufanya naye wimbo huo kabla hajawa maarufu, ila amesema amechukizwa na kiteno cha Cyril kutoa wimbo huo sasa, wakati yeye amekuwa maarufu zaidi chini ya WCB.