Jumamosi , 4th Apr , 2015

Nyota kutoka tasnia ya muziki wa Bongo Flava, Chin Beez amesema ana imani kuwa rekodi yake mpya itafika mbali kutokana na mapokezi makubwa iliyopata kutoka kwa mashabiki.

Chin Beez

Msanii huyo ambaye amerejea katika chati kwa kishindo na ngoma mpya inayokwenda kwa jina Pakaza, amemshirikisha mkali wa michano G Warawara kutoka kundi la Weusi.

Chin Beez katika mahojiano na eNewz amewataka pia mashabiki wake kufahamu kuwa, Video ya rekodi hiyo itakamilika ndani ya wiki hizi mbili, akiwa amempanga director Hanscana tayari kwaajili ya kazi hiyo.

Ikiwa pia hiki ni kipindi ambacho waamini wa dini ya kikristo wapo katika tafakari ya kifo cha Mkombozi wao Yesu Kristo kuelekea siku kubwa ya kufufuka kwake Pasaka Kesho, kwa niaba ya wasanii wengine, Chin Beez amewataka watu kusogea zaidi karibu na Mungu kutokana na mambo mengi ya kutisha na kukatisha tamaa kutokea katika kipindi hiki, yakihitaji imani thabiti ili kuyaelewa na kukabiliana nayo.

Staa huyo pia ametanguliza salamu zake za Heri ya Pasaka kwao kuelekea sikukuu ya Pasaka hapo Kesho.