
Chin Bees na Country Boy
Zogo hilo limefika hadi katika meza ya eNewz, baada ya Chin Bees kusema kuwa Country Boy hafikii levo zake kwa sasa na kwamba anapaswa ajilinganishe na wasanii wachanga wa Trap bongo, Country Boy amejibu mashambulizi hayo.
Country Boy 'Wiz' amesema, "Chin Bees ana tatizo na mimi, ananitafuta kwa sababu nafanya kazi ambazo zinaonekana zinamgusa, ni mdogo wangu nimemsaidia mimi katika 'game', hanifikii kwa kurap, kuvaa hata maisha", amesema Country Boy.
Pia Country Boy amesema kuwa alihusika katika kumsaidia Chin Bees kwenye kutambulisha ngoma yake ya kwanza.
Tazama hapa majigambo ya wote wawili.