Jumanne , 31st Mei , 2016

Baada ya stori kuzagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii dhidi ya rapa Chidi Benzi kutoroka Bagamoyo Sober House alipokuwa akipata matibabu baaada ya kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya sasa watu wa Sober House wamenyoosha maelezo.

Msanii wa Bongo Fleva Chidy Benzi

Akizungumza na eNewz mmoja wa wahusika wa Sober House ambae hakutaka kutajwa jina lake amesema, ikitokea Chidy atarudia kutumia dawa za kulevya tena basi wasimamizi wake ambao walimpeleka pale kwa mara ya kwanza watakuwa wamehusika kutokana na wao kushindwa kumtimizia ahadi walizokuwa wamempatia.

Aidha, ameongezea kuwa mteja ni kama mtoto mdogo ukimuahidi kitu basi lazima umtimizie lakini wao kushindwa kumuona alipokuwa akiwapigia simu kuwa anaumwa inawezekana ikawa ni sababu kubwa iliyomfanya Chidy kuondoka kwa kuwa alikuwa anaona wamemsusa ama wamemtelekeza ikiwemo na ahadi waliyokuwa wamempatia ya kumpeleka Italia kwa ajili ya matibabu zaidi.