Jumatano , 5th Mei , 2021

Mwimbaji wa nyimbo za injili wa Nigeria, Chidinma ameelezea kwanini alichukua uamuzi wa kuachana na muziki wa kidunia na kuhamia muziki wa injili.

Msanii Chidinma

Akizungumzia uamuzi huo wakati akitoa ushuhuda kwenye ibada moja kanisani, Chidinma amesema shetani amekuwa akishinda kwa muda mrefu maishani mwake lakini sasa anataka kutoa talanta zake zote kumfanyia kazi Baba yake aliye mbinguni.

Sipo hapa kwa sababu nataka kupata pesa, wala kwa sababu nataka umaarufu, nimekuwa navyo vyote hivyo na nadhani nimetosheka na yote hayo, kwa hiyo sasa hivi ni wakati wa kufanya kazi kwa baba yangu, Yesu anakuja hivi karibuni, mapema kuliko vile unavyotarajia”, amesema Chidinma.

Chidinma alipata umaarufu mkubwa kuanzia mwaka 2010, baada ya kushinda msimu wa tatu wa “Project Fame West Africa”, Jumapili ya Mei 2, 2021aliweka wazi kuachana na muziki wa kidunia na kurudi kwenye muziki wake aliowahi kuufanya wakati ana umri wa miaka 6 akiwa kanisani.