Chidi Benz amwambia ukweli Alikiba Harmonize na D

Jumanne , 20th Jul , 2021

Rapa Rashidi Abdallah Makwilo Chidi Benz 'King Kong' amesema anajua kwamba Alikiba, Diamond na Harmonize ndio wasanii wakubwa kwa sasa Bongo ila wajitahidi wawe na heshima.

Kutoka kushoto ni Chidi Benz, Harmonize, Alikiba na Diamond

Chidi Benz anasema wasanii hao wanatakiwa wawe na heshima ya ukweli ndani na nje pia waitumie vizuri mitandao yao ya kijamii sio kujiachia na kujisahau kisa wao ni mastaa.

"Hao ndio wasanii wakubwa, wanaosikika, wanaotamba, wana watu wengi kwenye mitandao yao na ndio wanaotuwakilisha wasanii wote, kitu ninachoweza kuwaambia na kuwashauri kwanza wawe na heshima ya ukweli, sio ile heshima wanapojua wanataka kampuni iwape pesa" ameeleza Chidi Benz 

Zaidi mtazame hapo chini kwenye video.