Jumatano , 22nd Jul , 2015

Msanii Jose Chameleone wa Uganda, ametoa kauli ya kutaka kuunganisha wasanii Bebe Cool na Eddy Kenzo, kuwataka kusimama na kusapotiana kwa kufuta uhasama unaoonekana kati yao.

msanii wa muziki wa nchini Uganda Jose Chameleone

Chameleone amewataka wasanii wenzake kuiga mfano wa wasanii kutoka Afrika Magharibi ambao wamekuwa wepesi kuonyesha sapoti na umoja katika ushindani nje ya mipaka yao, kauli inayopooza kughafilika kwa Bebe Cool kubezwa na mashabiki kwa kukosa tuzo ya kimataifa aliyokuwa anawania.

Kwa muda sasa Bebe Cool na Eddy Kenzo wamewekwa katika mizani na mashabiki, Bebe Cool akipigania heshima na ukongwe wake katika gemu, wakati Kenzo akiendelea kujivunia mafanikio na tuzo za kimataifa akiwa na kipindi kifupi tu katika tasnia ya gemu hiyo Uganda.