Ijumaa , 7th Mar , 2014

Msanii Jose Chameleone ameendelea kuandamwa na tuhuma za kuwa ndiye baba halisi wa binti wa mrembo 'video queen' Naila Salim, licha ya zoezi la kupima vinasaba lililofanyika hivi karibuni ili kujua ukweli wa sual

Mrembo Naila ambaye ametokea katika video ya Vumilia na Nkwagala Nyo ya msanii Chameleone, ameendelea kusisitiza kuwa, hakuwahi kujihusisha na mwanaume mwingine zaidi ya Chameleone hadi anapata ujauzito wa mwanae huyo licha ya majibu ya vinasaba kuthibitisha vinginevyo.

Bado haijafahamika ni hatua gani za ziada zitachukuliwa kuliweka sawa swala hili baina ya Naila na Chameleone ambaye kwa sasa ni baba halali wa watoto watano, wanne wakiwa ni kutoka ndoa yake na Daniella, na mmoja akiwa ni kutoka mpango wa kando na mpenzi wake wa zamani, Dorotia.