Alhamisi , 30th Jul , 2015

Mkongwe katika gemu Bwana Misosi ameweka mkakati mkubwa wa kurejea katika kilele cha chati za muziki wa Bongofleva ndani ya miezi miwili ijayo, akiwa na kazi na damu changa zinazofanya vizuri katika gemu kwa sasa.

staa wa miondoko ya bongofleva Bwana Misosi

Akiwa chini ya usimamizi wa Papaa Misifa ambaye ameiambia eNewz kuwa ana imani kubwa katika uwezo wa staa huyo, Misosi amesema kuwa ujo wake mpya utaenda sambamba na listening Party kwa wadau na mashabiki mbalimbali ili watoe maoni yao kutokana na nyimbo hizo mpya ambazo amefanya, zikiwemo kolabo na Jaguar, Makamua, Barnaba na wengineo wengi.