Jumatano , 28th Apr , 2021

Rapa aliyekuwa anamilikiwa na rekodi lebo ya Mdee Music chini ya msanii Vanessa Mdee aitwaye Brian Simba, amesema amemaliza mkataba wa kusimamiwa na lebo hiyo na hivi sasa yupo huru kufanya kazi zake mwenyewe.

Picha ya pamoja ya Brian Simba na Vanessa Mdee

Brian Simba amesema anamshukuru sana Vanessa Mdee kufanya nae kazo kwani amempa uzoefu mpya kwenye upande wa muziki pia amemfanya kuzunguka mikoa na nchi mbalimbali.

"Masomo hayajanirudisha nyuma yamenipa 'exposure' mpya kwenye maisha, kufanya kazi na Vanessa Mdee ilinisaidia vitu vingi kama kuzunguka mikoa na nchi mbalimbali, ilikuwa experience nzuri ila mkataba wetu wa kufanya kazi uliisha" amesema Brian Simba 

Pia amezungumzia kuhusu ujio wa Album yake mpya na uwepo wa wasanii wengine wapya wanaofanya muziki wa HipHop  kwa kusema  "Album yangu itatoka mwezi wa nane ina ngoma nyingi sana na kali, hapo katikati nilipokuwa shule walikuja marapa wengi wakali ila ni marafiki zangu wote, napenda wakali tuwe wengi".

Chanzo ni PlanetBongo ya East Africa Radio, Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 7:00 Mchana mpaka 10:00 Jioni.