Ijumaa , 27th Nov , 2015

Bobi Wine amezungumza ugomvi unaohisiwa kuwepo kati yake na Bebe Cool ambaye ni mshindani wake mkubwa katika tasnia ya muziki Uganda na kueleza kuwa binafsi hana muda wa kugombana na msanii huyo, zaidi ya kumrekebisha na kumkosoa pale anapokosea.

Bobi Wine | Bebe Cool

Bobi Wine ametolea mfano kuwa Bebe Cool ni msanii ambaye ana tabia ya kushambulia mashabiki katika mitandao, jukwaani na hata katika vyombo vya habari, tabia ambayo binafsi anaona sio sawa na ni lazima aikemee.

Upande wa Bebe Cool mpaka sasa haujazungumza lolote kuhusu Maneno hayo ya Bobi Wine yanayoonekana kuwa ni ya kichokozi yenye kuendeleza uhasama ambao unabaki dhahiri kati yao licha ya wasanii wenyewe kukana kutokuwa na maelewano wakati mwingine.