
Picha ya msanii Ben Pol na mkewe Anerlisa Muigai
Kupitia ukurasa wake wa Instagram taarifa hiyo inaeleza kuwa "Ben Pol angependa kuthibitisha uwepo wa shauri la talaka dhidi ya mke wake linaloendelea katika Mahakama ya mwanzo hapa Dar es salaam, Mahakama bado haijatoa talaka/maamuzi yoyote mpaka pale litakaposikilizwa na kukamilishwa"
"Masuala haya ni binafsi sana na kwa kuwa shauri linaendelea Mahakamani Ben Pol asingependa lizungumzwe zaidi kwa heshima ya pande zote na kwa kuheshimu kazi ya Mahakama"
Aidha imeendelea kueleza "Pia anaomba nafasi na faragha kwake na kwa familia katika kipindi hiki kigumu, anawashukuru wote kwa uelewa na pia kwa familia, marafiki na mashabiki wote kwa support mnayoendelea kuionesha".
Kuhusu chanzo cha Ben Pol kudai talaka hiyo Mahakamani bado hakijatajwa, wawili hao walifunga ndoa ya siri na picha za siku ya hurusi yao zilionekana Oktoba 2020.