Jumamosi , 28th Mar , 2015

Belle 9, msanii wa muziki wa kizazi kipya anayeiwakilisha poa Morogoro kupitia muziki wa kizazi kipya, anaingia katika orodha ya mastaa wa Bongo wanaounga mkono kampeni ya ZamuYako2015.

Belle 9

Belle 9 anafanya hivyo akiwa na ujumbe maalum kwa vijana kutokuchukulia poa suala zima la kujiandikisha kupiga kura na kutumia nafasi iliyopo mbele yao kushiriki kumchagua kiongozi wamtakae.

Belle 9 amesema kuwa, ni wakati wa vijana kuweka fikra zao katika uhalisia na kuamini kuwa inawezekana, na kuachana na kulalamika na kutumia njia zisizo halali kupambana na mifumo ya kisiasa inayowakwamisha kiuchumi.

Staa huyo siku ya jana pia ameachia rekodi yake mpya inayokwenda kwa jina Shauri Zao, ambayo ameifanya chini ya mtayarishaji muziki maarufu nchini, C9.

#ZamuYako2015