Jumanne , 14th Apr , 2015

Baada ya kuachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina Kukupenda, Msanii wa muziki Bee Man ambaye historia ya muziki wake imejengeka katika mahadhi ya tofauti, amesema kuwa anafanya hivyo kwa ajili ya kuwakilisha utamaduni na asili ya Tanzania.

msanii wa bongofleva Bee Man

Staa huyo amesema kuwa, kutokana na kukua kwa mitindo ya kunakili muziki hasa kutoka Afrika Magharibi, kwa upande wake ameamua kuangalia misingi ya wasanii wa zamani, wakiwepo wakina Baraka Mwinshehe walichokuwa wanakifanya, na kutembea katika misingi hiyo.