
Roma ameiambia Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa ataitisha mkutano na waandishi wa habari kutangaza rasmi kuwa taarifa za BASATA kuwa wimbo wake umefungiwa ni za uzushi na hazina ukweli wowote.
"Zilipokuja zile rumors za kwamba wimbo wa Roma umefungiwa, BASATA imefungia wimbo wa Roma, taarifa kama hiyo kila mtu anaipokea katika njia tofauti, Roma amekosea wapi, ama sheria za sanaa yetu zinamruhusu msanii aongee kitu gani na vitu kama hivyo, so miongoni mwa mashabiki zangu ni wanasheria tena wakubwa tu walio bobea ambao hiyo taarifa iliwasikitisha, ambao wanampenda Roma na pia wanaamini kuna uhuru wa kuongea katika nchi yetu, na hiyo inatokana kwamba hakukuwa na taarifa rasmi", alisema Roma.
Roma aliendelea, " kilichoamuliwa iliandikwa barua kuwahoji BASATA ni kwa nini wamefungia ngoma ya Roma hilo lilikuwa la kwanza, lakini la pili lilikuwa kama ni kweli je kuna sababu zozote ambazo zimepelekea nyinyi kufanya hivyo? kwa hiyo iliandikwa barua na ikatolewa siku tatu kwamba iwe wame reply ili sisi tuwe vizuri katika career yetu, kitu ambacho sasa hivi kimepita hata wiki mbili hakuna majibu yoyote, kwa hiyo tunaona bora tuite Press ije tufanye press comference tuwaambie watu nyimbo ya Roma haijafungiwa".
BASATA WAMJIBU.
Timu ya Planet Bongo haikuishia hapo na kuwatafuta wahusika wa Baraza la sanaa Taifa, na kumpata Katibu wa Basata Bwana Godfrey Lebejo ili kuthibitisha kama kweli walipokea barua hiyo, na kukiri kuwa waliipata barua hiyo na kwa nini hawajaijibu mpaka sasa.
"Ee naona alileta barua, aliweka kwenye mtandao, wao wenyewe waliiweka kwenye mtandao, tumeipokea, tumeipata na alikuwa ameipa Baraza siku mbili waweze kujibu na wala hatujaijibu.
kwa mujibu wa BASATA Roma aliiweka barua aliyoituma kwa baraza hilo kwenye mitandao, na ikumbukwe kwamba taarifa za kufungiwa kwa wimbo wake nazo alizipata kwenye mitandao, Planet Bongo ilipotaka kujua kwa nini BASATA hawajajibu barua hiyo na kujibiwa kuwa haina msingi.
"Kwa sababu alituletea barua tumeipokea, alitoa siku mbili, sasa hiyo ni sheria ya wapi, sijui kama anaweza kuchukua hatua nyingine anaweza akachukua hatua nyingine ya ziada, lakini haina msingi, sasa sijui vigezo gani anatumia vya namna hiyo, lakini barua tumeipokea na tumeipokea kama ilivyo kawaida barua zinapokelewa.