Baby John afunguka mazito kuhusu jinsia yake

Jumanne , 2nd Mar , 2021

Mwenyekiti wa Tanzania Voice of Humanity Baby John amesema kutokana na changamoto ukamilifu wa viungo vya uzazi wakati wa kuzaliwa kwake ndiyo vinafanya kushindwa kuitwa mwanamke au mwanaume.

Mwenyekiti wa Tanzania Voice of Humanity, Baby John

Akizungumza kwenye kipindi cha DADAZ ya East Africa TV Baby John  ameeleza kuwa hawezi kusema kama ana jinsia moja au mbili kwa sababu ili uwe una jinsia kama mwanaume au mwanamke lazima kuna baadhi ya viungo uwe navyo mwilini ambavyo yeye hana.

"Kwa kifupi nilizaliwa na changamoto ya ukamilifu wa viungo vya uzazi ambavyo vinafanya kushindwa kuitwa mwanamke au mwanaume, nilivyozaliwa mama yangu alipewa taarifa mbili ya kwanza ni mtoto wa kiume, ya pili wa kike"

"Siwezi nikasema nina jinsia mbili au moja kwa sababu ili uwe na jinsia kuna viungo lazima uwe navyo, kwa mfano mwanamke lazima awe na ovari, uteras na mirija ya uzazi lakini hivyo vyote mimi sina na kwa mwanaume pia hivyohivyo, nimebaki njia panda

Aidha ameongeza kusema watu wenye tatizo hilo huwa wanazaliwa hivyo na hawataweza kushika ujauzito wala kumpa mtu ujauzito.

Zaidi mtazame hapa chini