Alhamisi , 3rd Dec , 2015

Baby J, nyota wa muziki anayeiwakilisha Zanzibar Vizuri, amefanyia mkarekebisho makubwa muziki wake ikiwa ni sambamba na kuingia chini ya usimamizi wa Mkubwa na Wanawe.

nyota wa muziki anayeiwakilisha Zanzibar Jamila Abdullah aka Baby J,

Marekebisho hayo makubwa kwa diva huyo ni sambamba na matayarisho ya kuachia rekodi yake mpya inayokwenda kwa jina 'Ndoa'.

Baby J amewafahamisha mashabiki wake kuwa, Said Fella na Babu Tale ndio watakuwa wakiendesha kazi zake akiwa tayari kuanza na rekodi ya 'Ndoa' ambayo inagusia pia uzoefu wake binafsi katika mahusiano ya namna hiyo, kama anavyoeleza yeye mwenyewe hapa.