Alhamisi , 19th Mar , 2015

Msanii wa muziki Yemi Alade wa nchini Nigeria, ametangaza tarehe 7 mwezi Mei mwaka huu kuwa ndiyo siku ambayo marehemu baba yake, Kamishna Mstaafu J.A. Alade aliyefariki dunia tarehe 16 mwezi Januari atazikwa.

Msanii wa muziki wa nchini Nigeria Yemi Alade

Msiba wa baba wa star huyo utafanyika kwa siku mbili kwa taratibu za huko kwao Nigeria, kwa sasa Yemi mwenyewe akiwa anaendelea na shughuli zake za muziki ziarani huko barani Ulaya.

Star huyo kwa njia ya mtandao ameonesha kuwa msiba huo unaendelea kumgusa kwa kuandika kuwa, anamkumbuka mzee wake huyo kila siku, akiamini kuwa kwa sasa amepumzika kwa amani.