Jumanne , 19th Mei , 2015

Rapa Wangechi kutoka nchini Kenya, ameachia ngoma yake rasmi ya kwanza baada ya tukio la kunusurika kifo na kipindi kirefu cha kujiuguza majeraha ya ajali mbaya kabisa ya gari aliyoipata mwezi Oktoba mwaka jana.

msanii wa miondoko ya rap nchini Kenya Wangechi

Kuhusiana na rekodi hii aliyoipatia jina 'Cardiac Arrest', Wangechi amesema kuwa ni ngoma ya ukombozi ambayo inamfanya ajisikie vizuri baada ya kile kilichotokea, kusafisha moyo wake, rekodi ambayo imetengenezwa na prodyuza Kevin Provoke.

Staa huyo wa kike ameendelea kuwajulisha mashabiki wake juu ya maendeleo ya afya yake kwa njia ya mitandao ya kijamii, kwa sasa taratibu akiendelea kurejesha ratiba zake za maisha kama kawaida, ikiwepo shule na muziki wake.