Alhamisi , 18th Jun , 2015

AY asema kuwa kuna umuhimu wa kupunguza nafasi ya maamuzi ya kishabiki katika kazi za utoaji tuzo kwa waliofanya vizuri katika muziki

AY, nyota wa muziki anayeiwakilisha vizuri katika gemu ya muziki Bongo ametoa mtazamo wake juu ya namna ya kupunguza malalamiko na mkanganyiko katika vinyang'anyiro vya kuwasaka wasanii wanaofanya vizuri, na kueleza kuwa kuna umuhimu wa kupunguza nafasi ya maamuzi ya kishabiki kwa kuanzia.

AY amesema kuwa, anapendekeza mashindano haya kutoa asilimia 70% za maamuzi kwa paneli ya majaji, na 30% zilizobaki kuachiwa kwa mashabiki, hatua ambayo inaegemeza maamuzi ya mshindi katika vigezo zaidi.

Hapa the King of Commercial Hip Hop anaeleza kwa undani zaidi.