Jumanne , 17th Nov , 2015

Star wa muziki Avril wa Kenya, ameweka wazi kuwa taratibu za kuchunguza uhalali wa familia ya mchumba wake ambaye ni raia wa Afrika Kusini, ndio sababu inayochelewesha harusi yao mpaka sasa tangu mwezi wa 11 mwaka jana alipovishwa pete ya uchumba.

Staa wa muziki wa nchini Kenya Avril

Avril ameeleza kuwa, suala zima la harusi mara nyingi uhusisha wazazi zaidi, ambapo pale pande mbili zinapokubaliana hatua zinazofuata huenda vizuri, ufafanuzi ambao mwanadada huyo ameutoa katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni.

Kutokana na mchakato huo, Avril ambaye ameachia kazi mpya 'No Stress' akiwa amemshirikisha rapa AY na Muongoza Video Hanscana kutoka hapa Tanzania, amewaahidi mashabiki wake kuwa harusi hiyo itafanyika mwezi ujao.