Asha Boko
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Asha amesema anashangazwa na uchache wa wasanii wa kike kwenye upande wa Comedian na kuwataka wasiogope kwakuwa hakuna wasanii wa vichekesho Bongo wengi kwa upande wa wanawake.
Hata hivy amesema kwa sasa anampango wa kuachia movie zake peke yake hivyo anaomba sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki zake ili aweze kutambua kiwango chake cha kuigiza kwa sasa.