Jumanne , 5th Oct , 2021

Msanii Amber Lulu amefunguka kwamba lengo lake ni kupata watoto watano kwa baba tofauti kwa sababu hawezi kukaa na baba mmoja huenda akifariki atapata tabu akiwa peke yake.

Picha ya msanii Amber Lulu kwenye interview na East Africa TV

Amber Lulu ambaye kwa sasa ana mtoto mmoja na msanii Emba Bosion ameshea hilo kupitia EATV & EA Radio Digital baada ya kuulizwa mipango yake kuhusu watoto anaotaka kuwa nao.

Aidha amemtaja msanii Juma Jux kama ndio mtu anayetamani kupata naye mtoto kwa sababu ana akili, yupo smart na atamuongoza vyema pia amekuwa akimfuatilia msanii huyo kwa muda mrefu.