Katika orodha hiyo Amber Lulu amemtaja msanii wa kwanza ambaye hawezi kutoka naye ni Dudubaya, Ommy Dimpoz, Alikiba na wengine wengi.
Akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka kupitia kurasa za Facebook na YouTube za East Africa Television, Amber Lulu amesema, "siwezi kutembea na msanii kama Dudubaya anaongea sana, Kalapina yeye ni mkorofi sana, Ommy Dimpoz yeye hana habari na wanawake sijui kwanini".
Kwa sasa Amber Lulu anatamba na ngoma ya 'Haters' ambayo anatarajia kutoa video wiki ijayo.
Tazama mahojiano kamili hapo chini

