Jumatatu , 23rd Jun , 2014

Mkongwe kutoka sanaa ya muziki nchini Kenya, msanii Amani ameweka wazi kuwa yupo katika ratiba kali ya mazoezi katika kupambana na uzito mkubwa ambao uliongezeka mwilini kwake hususan katika kipindi cha mwisho wa mwaka uliopita.

Msanii wa nchini Kenya Amani

Amani ambaye amesema kuwa uzito wake huu umechangiwa na kula pamoja na kupumzika sana, na sasa anafanya zaidi mazoezi ya Yoga na kuhudhuria gym sambamba na kutembea wakati wa jioni ili kupunguza uzito na kukaa katika shepu makini.

Amani pia amekanusha taarifa za kuwa ujauzito ndio umechangia kwa yeye kuongezeka kama ambavyo tetesi zinazosambaa mtaani zimekuwa zikieleza.