Ijumaa , 18th Oct , 2024

Tarajia kukutana na ngoma ya pamoja kutoka kwa Msanii ALIKIBA pamoja na RAYVANNY siku za hivi karibuni.

 

Hii imekuja baada ya wawili hao kuonekana wakiwa studio pamoja jambo ambal limeaminisha mashabiki wa muziki wao kuwa wanarekodi wimbo pamoja.

Hii imeleta picha mpya kwenye kiwanda cha bongo fleva Tanzania, kuwaona wawili hao kuwa studio wakirekodi, ikilinganishwa na zile story za zamani za kuwa msanii fulani akiwa karibu na DIAMOND ni ngumu msanii huyo tena kuwa karibu na ALIKIBA.