Jumapili , 11th Dec , 2016

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa mwaka huu 2016 kampuni ya East Africa Television LTD kufanya tuzo zinazofahamika kama EATV AWARDS msanii Alikiba ameibuka kinara kwa kuzoa jumla ya tuzo tatu ambazo ni wimbo bora wa mwaka, video bora ya mwaka, mwanamuziki

Alikiba akiwa na tuzo zake alizojizolea leo

 

Akiongea wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Alikiba alisema yeye ni kama amewashikia tu mashabiki zake kwani tuzo hizo ni zao wao, hivyo aliwashukuru mashabiki kwa kumlinda na mambo mengi ikiwa pamoja na kumuwezesha kuibuka kinara katika tuzo hizo tatu.

"Napenda kuwashukuru sana waandaaji wa tuzo hizi East Africa Televison, napenda kuwashukuru mashabiki zangu maana ninyi mmekuwa mkinilinda kwa mengi, tuzo hizi naweza kusema ni zenu nyinyi na mimi ni kama nimewashikia tu, nashukuru kwa kuniwezesha kushinda tuzo hizi maana bila nyinyi mimi si kitu". Alisema Alikiba.

Alikiba amekuwa msanii wa kwanza katika tuzo za EATV AWARDS kuibuka na tuzo nyingi zaidi kwa upande wa wasanii wa muziki, ikumbukwe pia mwaka jana katika tuzo za Kilimanjaro Music Awards Alikiba alikuwa kinara kwa kujizolea tuzo tano.

Tags: