Jumapili , 15th Aug , 2021

Bondia Nico Ali Walsh, Mjukuu wa bingwa wa zamani wa uzito wa juu wa masumbwi duniani Muhammad Ali, ameshinda pambano lake la kwanza kwa knock out katika raundi ya kwanza, huku akiwa amevaa Bukta sawa na aliyokua akivaa Babu yake.

Bondia Nico Ali Walsh upande wa kulia

Bondia huyo wa uzito wa kati Ali Walsh ni mtoto wa Robert Walsh na Rasheda Ali Walsh, binti ya Muhammad Ali. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 21 hili ndio pambano lake la kwanza 'rasmi' lilofanyika katika jimbo la Oklahoma nchini Marekani.

Ali Walsh, aliyeamua kuvaa mavazi aliyotengenezewa babu yake katika miaka ya 1960, alimwangusha mpinzani wake katikati ya raundi ya kwanza kabla ya mwamuzi kusimamisha pambano hilo.