Ijumaa , 19th Sep , 2014

Msanii wa muziki Akon amekutana na Rais Uhuru Kenyatta huko jijini Nairobi Kenya, mkutano ambao umekuwa ni muendelezo wa mpango wa msanii huyu kusaidia miradi ya Umeme Afrika ambapo kwa Kenya utawafaidisha wakazi wa Kibera.

msanii wa muziki wa Senegal Akon akiwa na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Akon katika ziara hii pia ameandamana na mwenzi wake ambaye amefahamika kwa jina Unique, ambapo pia wanatarajia kufika nchini Congo kwaajili ya onyesho la kuhamasisha amani litakalofanyika siku ya Jumapili.

Hii ni mara ya pili kwa Akon kukutana na Mheshimiwa Kenyatta, ambapo hivi karibuni walikutana pia huko Marekani wakati wa mkutano mkubwa wa Marais wa Afrika na Rais Barack Obama.