msanii wa muziki wa nchini Senegal Akon
Kwa sasa msanii huyo mwenye asili ya Senegal amejipanga kwa ajili ya kujenga chuo huko Bamako, ambapo kitakuwa kikifundisha wataalam katika sekta hiyo ya umeme kwa ajili ya kuendeleza mradi huo kupitia mpango wake wa Akon Lights Africa.
Huu ni uwekezaji mkubwa kabisa ambao staa huyo wa muziki ameuanza kwa lengo la kutoa mchango wake kuendeleza bara hili ambalo ndilo asili yake, kutokana na mafanikio yake ya kimuziki.