Ijumaa , 9th Nov , 2018

Msanii wa Hiphop nchini na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Seleman Msindi amemfananisha Msanii wa bongofleva nchini Ali kiba na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete juu ya namna ambavyo wamekuwa wakikwepa mialiko mbalimbali wanayopewa.

Afande Sele, Jakaya Kikwete, Ali Kiba.

Afande Sele amedai wawili wao wamekuwa wakikataa kwa namna yake baadhi ya mialiko ambayo wamekuwa wakipewa na baadhi ya wenzao ambao ni ,maarufu akitolea mfano Rais Mstaafu Kikwete kutoonekana kwenye baadhi ya shughuli ambazo Rais Magufuli anazungumza.

Afande Sele amesema "kitendo na sabbu za Ally Kiba kukwepa kiaina mualiko wa matamasha nchini kinafanana na sababu za Rais mtaafu Kikwete kukwepa kiaina maeneo mengi ambayo Rais Magufuli anahutubia licha ya marais wenzake wastaafu Mwinyi na Mkapa huwa wanakuwepo."

Aidha amesema "kwa watu wanaoelewa wanajua pamoja na kuwepo sababu nyingine nyingi zinazotolewa kuhusu huo ukwepaji wao mialiko wa 'kiaina' lakini sababu kuu na ya msingi ni uungwana walionao hawa wawili."

"Labda unadhani Kikwete anajisikiaje pale JPM anapoongelea vyeti feki, mishahara hewa, ujangili wa kuua wanyama hadi wengine kupandishwa kwenye ndege, ufisadi serikalini hadi kuua mashirika ya umma kama Reli, Ndege vingi vilifanyika kwenye utawala wake," ameongeza Afande Sele.
--