Jumamosi , 17th Mei , 2014

Msanii maarufu wa maigizo na muongozaji wa filamu za Kitanzania, Adam Philip Kuambiana, amefariki dunia ghafla asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam.

Marehemu Adam Philip Kuambiana

Akizungumza na EATV mwenyekiti wa Bongo Movies, Steve Nyerere, amesema Adam Kuambiana amefariki wakati wakiwa "Location", wakiandaa filamu.

Mwili wa msanii huyo, umepelekwa katika hospitali ya Muhimbili, kwa uchunguzi zaidi