Pato la Taifa lakuwa kwa asilimia 6.9

Alhamisi , 8th Apr , 2021

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema tathimini za utekelezaji wa mpango wa pili wa maendeleo ya  taifa limeonesha kuwa pato la taifa lilikuwa kwa asilimia 6.9.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba

Dkt.Mwigulu amesema hayo akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa Mpango wa  wa tatu wa maendeleo ya taifa wa miaka mitano ambapo amesema mpango huo una lengo la kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu.

“Kuhusu tathimini na utekelezaji mpango wa maendeleo ya taifa  uliopita inaonesha kuwa katika kipindi cha utekelezaji cha miaka minne pato la taifa lilikuwa kwa 6.9%  mfumuko wa bei ulikuwa wa wastani 4.1%  kwa mwaka, ikiwa ndani ya lengo la kutozidi asilimia 5,” amesema Dkt.Mwigulu

Awali kabla ya kuwasilisha mapendekezo hayo Dkt. Mwigulu alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uteuzi katika nyadhifa aliyompa na kusema kuwa uteuzi huu unadhihirisha Rais ana imani kubwa na wana yanga

“Mhe. Spika uteuzi wa Makamu wa Rais na uteuzi wangu umeonyesha Mhe. Rais ana imani kubwa sana na wana yanga hasa ukizingatia historia ya ukombozi wa taifa hili," amesema Dkt.Mwigulu