Dkt.Mpango atembelea kituo cha Huruma

Jumatatu , 5th Apr , 2021

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amelishukuru Shirika la Teresia wa Mtoto Yesu lenye Makao Makuu yake Nchini india kwa kazi nzuri wanayoifanya kuisaidia Tanzania  katika kazi ya kuwatunza Watoto Yatima, Wazee na Watu wenye Mahitaji maalUM.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akifurahia jambo na Mtoto anaelelewa na kutunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango ameyasema hayo leo April 05,2021 katika Kituo cha Kuwatunza Watoto Yatima, Wazee pamoja na Watu wenye Mahitaji Maalum cha Huruma Missionary Sisters of charity kiliopo Hombolo jijini Dodoma.

Aidha Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amesema atawahimiza Wizaya ya Afya na Maendeleo ya Jamii kitengo cha Ustawi wa Jamii wafike katika Kituo hicho waweze kufanya kazi ya kutoa huduma Zaidi.

Kituo hicho kinachotunza Watoto Yatima, Wazee, pamoja na Watu wenye Mahitaji Maalum kina Jumla ya Watu 90 wenye Uhitaji wa aina mbalimbali.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amefika katika kituo hicho kwa ajili ya kuwafariji pamoja na kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo Chakula, Sabuni, Vinywaji