Jumatano , 20th Dec , 2017

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amekiponda Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushindwa kumpata Spika wa Bunge la Afrika Mashariki kwa kuzidiwa ujanja na wabunge wa Rwanda na Uganda, kwa madai kwamba wameshindwa kuichakachua.

Heche amesema hayo ikiwa ni baada ya CCM kumuweka mgombea wake kuwania nafasi ya uspika wa bunge la Afrika Mashariki (EALA) Adam Kimbisa ambaye baadaye aliambulia kura 0.

"Ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huwezi, CCM wamejaribu kutaka kuchakachua hadi Afrika Mashariki wamesahau kwamba kule kuna wachakachuaji wenzao kutoka NRM, RPF" Heche.

Heche ameongeza kwamba "CCM hadi Afrika Mashariki wanataka kuiba kitu ambacho sio hali yao!!! Wamekutana na wachakachuaji wenzao kutoka Rwanda na Uganda wakasalimu amri inatia aibu na doa kwenye heshima ya nchi'.

Hata hiyo taarifa iliyotolewa juzi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilikosoa kitendo cha CCM kuweka mgombea wake kwenye nafasi ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki kwa madai kwamba haikutakiwa kufanywa hivyo kwani ilikuwa zamu ya Rwanda kushika nafasi hiyo, na kusema kwamba kitendo hicho kitasababisha mgogoro wa kidiplomasia.

Pamoja na hayo Mgombea Martin Ngoga wa Rwanda jana ameapishwa kuwa Spika mpya wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) baada ya kuchaguliwa kwa Kura 35, akifuatiwa na Leontine Nzeyimana wa Burundi aliyepata Kura 1 huku Adamu Kimbisa wa Tanzania akiambulia 0