
Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson ameitaka Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano kutoa taarifa Bungeni juu ya suala hilo.
Akielezea hoja hiyo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani amesema kwamba zoezi hilo lipo pale pale kwa kuwa simu feki zina madhara kwa watumiaji.
‘’Simu feki ni lazima zizimwe Juni 16 kwa kuwa zina madhara ya kiafya na kiusalama kwa watumiaji’’ Amesema Naibu Waziri Ngonyani.
Kwa muda wa miezi kadhaa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA imekuwa ikitoa elimu kwa umma juu ya uzimwaji wa simu feki nchini Juni 16 2016 kwa lengo la kuwalinda watumiaji kiafya na kiusalama.