
Inakadiriwa kuwa watu 46,499,537 wanasifa ya kushiriki upigaji kura katika zoezi hilo kwa mujibu wa takwimu za wapigakura wa UK.
Zoezi hili la kura ya maoni ni la tatu kwa mataifa ya UK kufanyika kitaifa katika historia, na linakuja baada ya kampeni za miezi minne baina ya wanaotaka wajitoe na wanaotaka wabakie katika Umoja wa Ulaya.
