Ijumaa , 23rd Sep , 2022

Taasisi ya Mifupa MOI, imetoa tahadhari kwa jamii juu ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la wagonjwa wanaopata kiharusi, ambapo kwa mwezi mmoja pekee wanapokea zaidi ya wagonjwa 30 wakiwa tayari wamepata ugonjwa huo.

Taasisi ya Mifupa MOI

Mkurugenzi wa upasuaji ubongo na mishipa ya fahanu MOI Dkt Laurent Mchome, amesema ugonjwa wa kupooza unaoongoza kwa kuwapata wananchi hasa wenye umri wa kuanzia miaka 40 ni damu kumwagikia ndani ya ubongo kutokana na mifumo ya mishipa ya damu  kushindwa kupitisha damu kutokana na mafuta mengi mwilini.

Amesema kama Watanzania hawatabadilisha aina ya maisha ikiwemo ulaji wa vyakula visivyo na uhai kwenye mwili tatizo hilo la watu kupooza mwili litaendelea kuwa kubwa na taasisi hiyo inaweza ikazidiwa na wagonjwa wa aina hiyo