
Shirika la misaada la Walking Borders linasema boti hiyo ya uvuvi ilisafiri kutoka Kafountine, mji wa pwani kusini mwa Senegal ambao uko takriban kilomita 1,700 kutoka Tenerife.
Kundi hilo linasema watoto wengi walikua ndani ya boti hiyo, shirika la habari la Efe nchini Uhispania limeripoti.Boti mbili zinazofanana na hizo zilizobeba watu wengine kadhaa pia zinasemekana kupotea.Idara ya uokoaji baharini nchini Uhispania imeiambia Efe kuwa ndege moja ilijiunga na msako huo.
Boti hiyo iliyokuwa na watu 200 iliondoka Kafountine tarehe 27 mwezi Juni, ikielekea visiwa vya Canary. Kuna wasiwasi idadi ya watu waliotoweka katika boti kufikia zaidi ya 300 sababu ya kukosekana kwa taarifa sahihi.