Ijumaa , 17th Jun , 2016

Kampuni ya Reli nchini Tanzania TRL kumwaga kokoto katika njia ya treni ili kukabiliana na vumbi.

Zaidi ya Shilingi Milioni 700 zimetengwa na kampuni ya reli nchini Tanzania (TRL) kwa ajili ya kumwaga kokoto katika maeneo ambayo njia ya treni ya abiria inafanya safari zake ili kuweza kupunguza vumbi ambalo lilionekana kuwa kero kwa wakazi wa maeneo ya jirani na njia hiyo..

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa TRL Bw Masanja Kadogosa amesema kuwa kwa muda mrefu wananchi hasa wa maeneo ya kati ya Ubungo maziwa mpaka Posta wamekuwa wakilalamikia kampuni hiyo kuwa treni hilo hutimua vumbi jingi na kusababisha maradhi kama mafua na kifua.

Aidha Bw Kadogosa amewataka wakazi wa maeneo hayo kutunza miundombinu ya njia hiyo kwani kumekuwepo na watu wachache wasiowaaminifu ambao wanachukua kokoto zilizoshikilia njia ya reli na kwenda kuuza.

Kwa upande wao wakazi wa eneo la buguruni kwa mnyamani wamepongeza juhudi za serikali katika kutatua kero hiyo ya vumbi kwa kumwaga kokoto na wanaahidi watakuwa walinzi kwa wenzao waasiowaminifu waliogeuza mawe hayo kuwa mtaji.