Jumamosi , 13th Jul , 2024

Idadi ya watoto wanaoathirika na tatizo la moyo imetajwa kuzidi kuongezeka nchini ambapo kwasasa takwimu zinaonesha katika kila watoto 100 wanaozaliwa kuna uwezekano mtoto mmoja mpaka watoto nane wanazaliwa wakiwa na tatizo la moyo 

Idadi ya watoto wanaoathirika na tatizo la moyo imetajwa kuzidi kuongezeka nchini ambapo kwasasa takwimu zinaonesha katika kila watoto 100 wanaozaliwa kuna uwezekano mtoto mmoja mpaka watoto nane wanazaliwa wakiwa na tatizo la moyo 

Ambapo kutokana na familia nyingi kuwa na hali duni nchini Tanzania wengi wao wanashindwa kumudu gharama za matibabu ya moyo kwa watoto ambapo wito umetolewa kwa wananchi mmoja mmoja au taasisi kujitokeza kuchagia matibabu hayo kwasababu zaidi ya watoto 50 kwa kipindi cha miezi mitatu wameshindwa kumudu gharama na wanahitaji msaada ili kupata matibabu ikiwemo upasuaji 

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya moyo ya Jakaya kikwete (JKCI) Dkt Selende Kubhoja anasema tatizo la moyo limezidi kuongezeka siku baada ya siku kwa watoto ambapo amesema kuna uwezekano zaidi ya watoto 2000 wanazaliwa wakiwa na tatizo la moyo Tanzania 

"Kutokana na mifumo ya maisha watoto wengi kwasasa huzaliwa wakiwa na matatizo ya moyo wapo ambao wamezaliwa wakiwa na matundu kwenye moyo na wengine moyo kuwa mkubwa hali inayowalizimu kuhitaji matibabu ambayo pia ni gharama kubwa"
 
Amesema Katika kuwapa matibabu watoto wenye matatizo ya moyo changamoto kubwa imesalia kuwa gharama ambapo yapo matatizo yanayotibiwa kwa zaidi ya milioni 8 mpaka 30 ambazo mwananchi wa kawaida si rahisi.