Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modest Kipilimba akijitambulisha kabla ya kuanza kikao cha Watendaji Wakuu wa NIDA.
Akiongea jana Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dkt. Modest Kipilimba amesema pia wafanykazi 802 wa kudumu watafanyiwa tadhimini ya utendaji wao wa kazi na huenda wafanyakazi wengine watarudishwa utumishi ambako watapangiwa kazi nyingine.
Dakta Kipilimba amesema kuwa Mamlaka imekuwa ikizalisha vitambulisho 1200 kwa siku badala ya vitambulisho 24000 kwa siku jambo ambali ni sawa na uzalishaji wa wa chini ya asilimia kumi hivyo kuisabishia hasara mamlaka hiyo.
Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa katika uboreshaji wa utoaji wa vitambulisho hivyo wameongea na tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),ambao wamekubali kuwapatia mashine 5000,ambazo zilikuwa zinafanyiwa matengenezo.
Amesema kuwa mashine hizo zitasaidia kuongeza kasi ya kufikia wananchi wengi zaidi na kuwapatia vitambulisho lengo ikiwa ni kuhakikisha watanzania wote wanakuwa na vitambulisho vya taifa.