
Jenerali Li hajaonekana hadharani kwa takriban wiki mbili na ameripotiwa kukosa mikutano kadhaa.
Kutokuwepo kwa bwana Li kunafuatia hatua za hivi karibuni za maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wa jeshi. Alipoulizwa kuhusu hali ya Li katika mkutano wa kawaida na waandishi wa habari Ijumaa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning alisema "Sijui hali ilivyo."
Maswali kuhusu mahali Li alipo yanafuatia kutoweka kwa Qin Gang, ambaye aliondolewa madarakani kama waziri wa mambo ya nje wa China mwishoni mwa mwezi Julai baada ya kutoonekana hadharani kwa mwezi mmoja.
Katika tovuti za serikali ya China na jeshi, Li bado ameorodheshwa kama waziri wa ulinzi, diwani wa jimbo na mjumbe wa Tume ya Kijeshi ya Kati ya chama hicho (CMC).