Watumishi wa Wizara ya Maliasili na utalii
Akielezea tuzo hiyo ya banda bora na mashuhuri category ya Wizara na Taasisi, Mwenyekiti wa Maonesho ya Sabasaba Wizara ya Maliasili na Utalii, Filex John, amesema ni matokeo chanya ya uongozi mzuri wa Wizara hiyo pamoja na kazi iliyofanywa na watumishi wa Wizara hiyo ya utoaji huduma kwa kiwango cha juu kwa wote waliofika kwenye banda hilo.
John amewashukuru wadau na wananchi wote waliojitokeza kupata huduma kwenye banda hilo la Maliasili, pamoja na ushirikiano waliotoa katika kuhakikisha maonesho hayo yanakuwa na mafanikio makubwa.