
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI anayeshughulikia afya, Dkt. Deo Mtasiwa (mwenye tai) akiwa na mwenyekiti wa tume ya kudhibiti ukimwi TACAIDS, Dkt Fatma Mrisho
Hayo yameelezwa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) anayeshughulikia afya, Dkt. Deo Mtasiwa, wakati akifungua mkutano wa wadau wa afya kutoka tume ya kikristo ya huduma za jamii nchini (CSSC) uliokuwa ukijadili namna ya kuboresha elimu katika vyuo vinavyotoa elimu ya afya.
Aidha Dkt. Mtasigwa amesema serikali inakabiliwa na uhaba wa watumishi wapatao elfu 42 katika sekta ya afya, ambapo kwa sasa tayari imeshatangaza nafasi elfu 11 ili kupunguza uhaba huo.